Matthew 15:21-26

21 aIsa aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. 22 bMwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana.”

23Lakini Isa hakumjibu neno. Hivyo wanafunzi wake wakamwendea na kumsihi sana, wakisema, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele.”

24 cIsa akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea.”

25 dLakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Isa, akasema, “Bwana, nisaidie!”

26Isa akajibu, “Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

Copyright information for SwhKC